28/07/2026
Al-Basira kutoka katika Vitabu vya Ahlus-Sunnah 13
Kuondoa mashaka katika kuthibitisha kwamba Ahlul-Bayt ni kinga na usalama kwa Ummah
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
{Na Yeye ndiye aliyekujaalieni nyota ili miongozwe nazo}.
(Sura Al-An‘am: 97)
Je, ni akina nani hao “nyota” ambao tunaongozwa nazo? 🤔
Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema:
"Nyota ni kinga kwa watu wa mbinguni; zitakapoondoka, yatawafikia yale waliyoahidiwa. Na mimi ni kinga kwa Maswahaba wangu maadamu niko pamoja nao; nitakapoondoka, yatawafikia yale waliyoahidiwa. Na Ahlul-Bayt wangu ni kinga kwa Ummah wangu; watakapoondoka Ahlul-Bayt wangu, yatawafikia yale waliyoahidiwa."
(Al-Mustadrak ‘ala al-Sahihayn, Hadithi Na. 3721. Al-Hakim amesema: Isnadi yake ni sahihi).
Na pia amesema:
"Nyota ni kinga kwa watu wa ardhini kutokana na kuzama (majini), na Ahlul-Bayt wangu ni kinga kwa Ummah wangu kutokana na mifarakano. Ikiwa kabila lolote miongoni mwa Waarabu litapingana nao, watagawanyika na kuwa kundi la Shetani."
(Al-Mustadrak ‘ala al-Sahihayn, Juz. 3, Uk. 162. Al-Hakim amesema: Isnadi yake ni sahihi).
Na Aisha, Talha, Zubair na Muawiya walipingana na Ahlul-Bayt (a.s). Na yeyote anayepingana nao huwa katika kundi la Shetani. Wala hawafuati kundi la Shetani isipokuwa mashetani.