09/03/2026
Iran imerusha makombora yake ya kwanza kuelekea Israeli leo Jumatatu March 09 2026 tangu kuteuliwa kwa Kiongozi Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei. Tukio hili linaonekana kuwa hatua ya kwanza ya kijeshi chini ya uongozi wake mpya na linaashiria kuendelea kwa mvutano mkali kati ya Iran dhidi ya Israel pamoja na mshirika wake mkubwa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha serikali ya Iran IRIB, jeshi la Iran lilifyatua wimbi la kwanza la makombora kuelekea maeneo yaliyokaliwa na Israel k**a sehemu ya kile kinachoelezwa kuwa operesheni ya kulipiza kisasi na kuonyesha uwezo wa kijeshi wa taifa hilo. Kituo hicho kimechapisha pia picha ya kombora moja likiwa limeandikwa maneno ya kauli mbiu inayosema Kwa Amri Yako Sayyid Mojtaba jambo linaloashiria kuwa mashambulizi hayo yanafanywa chini ya maelekezo ya moja kwa moja ya Kiongozi Mkuu mpya wa Iran.
Wachambuzi wa masuala ya siasa na usalama wa kimataifa wanasema hatua hiyo inaweza kuongeza zaidi mvutano katika eneo hilo kwa sababu ni mara ya kwanza kwa Iran kufanya shambulizi kubwa la aina hiyo tangu Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei achukue rasmi nafasi ya uongozi wa juu wa kidini na kisiasa nchini humo. Mashambulizi hayo pia yanaonekana k**a ujumbe kwa Israel pamoja na washirika wake kwamba sera za kijeshi za Iran hazitabadilika licha ya mabadiliko ya uongozi.
Wakati hali hiyo ikiendelea Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ametoa wito wa kupunguzwa kwa kiwango cha mapigano katika eneo la Mashariki ya Kati. Akizungumza katika mahojiano na kituo cha habari cha Sky News amesema nchi za Ghuba zina wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kwa vita hivyo kwa sababu vinaweza kuathiri usalama wa eneo zima pamoja na shughuli za kiuchumi.
Amesema mataifa ya Ghuba hayakutarajia kuona mashambulizi yakifanywa na jirani yao Iran kuelekea nchi za eneo hilo au maeneo yaliyo karibu nao.