Yaa Mussa Poultry Farm

Yaa Mussa Poultry Farm Idle Mind is a workshop of The Devil

✍️🐓 YAJUE HAYA👇 ILI UANZE KUFUGA KUKU🐓 SASA.✍️Ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli muhimu katika sekta ya kilimo ambayo i...
17/05/2024

✍️🐓 YAJUE HAYA👇 ILI UANZE KUFUGA KUKU🐓 SASA.✍️

Ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli muhimu katika sekta ya kilimo ambayo inaweza kuleta faida kubwa kwa mkulima. Kuku wanaweza kufugwa kwa ajili ya nyama, mayai, na hata k**a biashara ya kuuza vifaranga na kuku wazima. Hapa kuna hatua muhimu katika ufugaji wa kuku:

1. ✍️Uchaguzi wa Aina ya Kuku✍️ Chagua aina ya kuku ambayo inafaa na inayostahimili mazingira yako. Kuna aina za kuku za nyama, mayai, na za kienyeji.

2. ✍️Mazingira Bora ya Kuku✍️ Hakikisha unaandaa banda zuri ambalo linatoa ulinzi dhidi ya wadudu, wanyama waharibifu, na hali mbaya ya hewa.

3. ✍️Lishe Bora ya Kuku✍️ Hakikisha kuku wanapata chakula bora chenye lishe kamili kulingana na umri wao. Unaweza kuwapa malisho ya kibiashara au kujitengenezea mchanganyiko wako wewe mwenyewe.

4. ✍️Usafi na Afya ya Kuku✍️ Hakikisha banda la kuku linakuwa safi kila wakati na pia kufanya chanjo kulingana na ratiba ili kudhibiti magonjwa.

5. ✍️Uzalishaji Bora wa Mayai✍️ Ili kuhakikisha uzalishaji bora wa mayai, hakikisha kuku wana maji safi ya kutosha, wanapata lishe bora, na wanapata mazingira mazuri ya kuishi.

6. *✍️Uzalishaji wa Kuku wa Nyama✍️ Kwa kuku wanaolenga kwa ajili ya nyama, hakikisha wanapata chakula bora, wanakuwa na nafasi ya kutosha, na unawapeleka kwa wataalamu wa afya ya mifugo mara kwa mara.

Kuweka mkazo kwenye afya, lishe bora, na mazingira mazuri kwa kuku zako ni muhimu sana kwa mafanikio ya ufugaji wa kuku. Kumbuka pia kufanya tafiti zaidi au kuongea na wataalamu wa kilimo ili kupata ushauri zaidi kuhusu ufugaji wa kuku.k

NB: Usisahau ku SHARE na ku LIKE page yetu ya Yaa M***a Poultry Farm ili kujua mambo mbalimbali yanayohusu ufugaji wa kuku.

✍️KWANINI TUFUGE KUKU...? ✍️ Tuanze Na Swali... "Kwa Mfano Ikatokea Wafugaji Wote Wa Kuku Tanzania Tukaacha Kufuga Kuku ...
06/05/2024

✍️KWANINI TUFUGE KUKU...? ✍️

Tuanze Na Swali...
"Kwa Mfano Ikatokea Wafugaji Wote Wa Kuku Tanzania Tukaacha Kufuga Kuku Kitu Gani Kitatokea Katika Maisha Yetu Ya Kila Siku...?"

Majibu Yanayokujia Kichwani Kwako Basi Hayo Yote Ni Miongoni Mwa Sababu Za Kwanini Unatakiwa Ufuge Kuku...

✍️Kabla Ya Kuanza Kuelezea Kwanini Unatakiwa Ufuge Kuku. Unatakiwa Ujue Faida Za Kuku Katika Maisha Yetu Ya Kila Siku...

K**a Ulikua Unamchukulia Kuku Ni Kiumbe Wa Kawaida Tu Bhasi Tambua Kuku Anafaida Zifuatazo Katika Maisha Ya Binadamu...👇👇👇

1️⃣Nyama Ya Kuku Inapendwa Sana Kuliko Nyama Yoyote Ile Duniani...

2️⃣Ni Nyama Yenye Protini-Vitamini Na Madini.

3️⃣Nyama Ya Kuku Inasaidia Kuzuia Magonjwa Mbalimbali Katika Miili Yetu.

4️⃣Nyama Ya Kuku Inatumika Katika Diet Ya Kupunguza Uzito...

5️⃣Inasaidia Wale Watu Wasiotakiwa Kula Nyama Nyekundu..

✍️Baada Ya Kujua Faida Za Nyama Ya Kuku. Sasa Turudi Kwenye Swali Letu La Kwanini Ufuge Kuku...???

✍️Bila Kupoteza Muda Zifuatazo Ni Sababu Zinazofanya Wewe 🫵 Ufuge Kuku...👇👇👇

1️⃣Kuendeleza Uzao Wa Kuku...

✍️Hawa Kuku Tunaowaona Leo Ni Uzao Toka Enzi Za Mitume Na Mababu Zetu Wa Zamani Kwahiyo Kutokana Na Wao Walifuga Kuku Ndio Imetusaidia Leo Hii Kuwakuta Kwahiyo Ili Uzao Uzidi Kuendelea Na Sisi Tuliopo Leo Tunajukumu La Kuwa Wafugaji Wa Kuku...

2️⃣Mahitajio Makubwa Ya Nyama Na Mayai Ya Kuku...

✍️Maisha Yetu Ya Kila Siku Yanahitaji Uwepo Wa Kuku Ili Tuweze Kupata Kitoweo Pamoja Na Mayai Yake Kwahiyo Tambua Usipofuga Wewe Jamii Itapata Changamoto Ya Kupata Hivyo Vitu Kwahiyo Tunakuomba Ufuge Ili Kutatua Changamoto Ya Upatikanaji Wa Nyama Ya Kuku Pamoja Na Mayai...

3️⃣Changamoto Za Ajira Katika Nchi Yetu...

✍️Serikali Haiwezi Ajiri Watu Wote Kutokana Na Sababu Zilizopo Nje Ya Uwezo Wao Kwahiyo Kumekua Na Kundi Kubwa La Vijana Mtaani Ambao Hawana Shughuli Yoyote Ya Kufanya Kutokana na Hiyo Hali Unatakiwa Ujipange Kufanya Ufugaji Kwasababu Kuku Ni Biashara Na Pia Kuku Ni Ajira Kuliko Kukaa Tu Vijiweni Na Kupoteza Muda Wako Ni Kheri Ukawa Mfugaji Itakusaidia Kupata Pesa...

4️⃣Kuku Pekee Ndio Mfugo Unaofugwa Na Watu Wote...

✍️Kwa Kumalizia Somo Letu Tambua kuwa Kuku Ndio Mfugo Ambao Unaweza Kufugwa Na Watu Wote Yaani Wale Wenye Vipato Vikubwa, Wenye Vipato Vya Kati Na Wale Wenye Vipato Vya Chini Kabisa Kutokana Na Hii Sababu Ndio Maana Tunakushauri Ufuge Kuku Kulingana Na Kipato Ulichonacho Ili Ujikwamue Katika Hali Uliyonayo Kwasasa...

✍️Tunapenda Kuwa Wafugaji Ila Wengi Hatujui Kwanini Tunapaswa Kuwa Wafugaji Wa Kuku Tunaamini Kupitia Somo Hili Kuna Vitu Umejifunza...

✍️Anza Na Ulichonacho Usisubiri Mpaka Uwe Na Kingi Ndio Uanze Ufugaji Utachelewa Sana Kuanza...

🗣️NB: "Usisahau kushare na kulike page yetu ya Yaa M***a Poultry Farm ili tusambaze maarifa kwa watu wwngi."🗣️

Lets go farmers
04/05/2024

Lets go farmers

Idle Mind is a workshop of The Devil

Hello wapendwa.Napenda kuwakaribisha kwenye ukurasa huu ili tuweze kujuzana na kuelezana mambo mbalimbali yanayohusu ufu...
04/05/2024

Hello wapendwa.
Napenda kuwakaribisha kwenye ukurasa huu ili tuweze kujuzana na kuelezana mambo mbalimbali yanayohusu ufugaji, hasa ufugaji wa kuku kibiashara. HAKIKA KUKU NI BIASHARA.

Yaa M***a Poultry Farm ni page yetu sote.

Address

Chamazi Bamia
Dar Es Salaam
BAMIACHAMAZI

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yaa Mussa Poultry Farm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Yaa Mussa Poultry Farm:

Share