29/03/2026
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HUJAANZA UFUGAJI KUKU
Kabla hujaanza ufugaji wa kuku, kuna mambo muhimu ambayo kila mfugaji anapaswa kuyazingatia ili kuepuka hasara na kuhakikisha biashara yako inafanikiwa:
1. Chagua aina sahihi ya kuku Je, unataka kienyeji, broiler, au improved? Kila aina ina malengo tofauti.
2. Jua soko lako Hakikisha unajua wateja wako na bei nzuri ya kuuza mayai au kuku mzima.
3. Bajeti na gharama – Andika bajeti yako kwa kina, ukijumlisha chakula, dawa, chanjo, na ujenzi wa banda.
4. Banda bora – Banda lazima liwe safi, lenye hewa nzuri, na linazuia magonjwa.
5. Vyakula na malisho mbadala – Jua jinsi ya kuchanganya vyakula na kutumia vyakula mbadala k**a Azola na Funza kupunguza gharama.
6. Chanjo na dawa za kuku – Jua ratiba ya chanjo na dawa muhimu ili kuzuia magonjwa.
7. Maji safi na usafi – Kuku wanahitaji maji safi kila wakati; usafi wa banda ni kipaumbele.
8. Ratiba ya ufugaji – Pangilia kila hatua kuanzia kununua vifaranga, lishe, chanjo, hadi mauzo.
Kumbuka: Ufugaji bila maandalizi unaleta hasara. Anza kwa maarifa, plan nzuri, na utayari wa kushughulikia changamoto.
:-Karbu ufuge na Tumwesige Mixed Farm +255714887774