14/03/2022
MIUJIZA YA BINZARI MANJANO KATIKA KUBUSTI UZALISHAJI WA KUKU NA KUTIBU MAGONJWA
Wengi tunafahamu binzari ya manjano k**a kiungo muhimu kwenye mboga hasa nyama, pilau na biriani kinacholeta ladha tamu na mwonekano mzuri wa chakula. Binzari ya manjano pia ikiwekwa katika maharage inanoga sana na inabadilisha rangi na kuwafanya watoto wasiopenda maharage wavutiwe kula.
Lakini je, unajua binzari hii inaweza kufanya miujiza mikubwa katika matibabu ya magonjwa mengi ya kuku na kubusti uzalishaji wao wa nyama na mayai?
K**a haujui, basi upo unasoma eneo sahihi. Baada ya dakika 5 za kusoma hapa utakua mtaalamu wa kutumia binzari ya manjano kufanya miujiza ya uponyaji. Ahahahahah
Binzari ya manjano kitaalamu inajulikana k**a Curcuna Longa inatibu magonjwa mengi na kuchochea uzalishaji wa kuku. Leo nitakwambia jinsi binzari inavyotibu vidonda na magonjwa yanayopelekea kuku kupata vidonda.
Kuku wanapata vidonda kupitia kudonoana, kukatwa, kuchomwa au kukanyaga kitu chenye ncha kali, kung'atwa na wanyama au wadudu, kuvimba nyayo na miguu (Bumblefoot) na ndui ya kuku.
Matatizo haya yote kiboko yake ni binzari ya manjano. Leo kwa sababu ya muda nitakwambia tu kuhusu Bumblefoot.
Kwa tatizo la Bumblefoot unatakiwa kwanza kusahihisha makosa uliyofanya kabla haujatibu ugonjwa. Kuku wako wamevimba nyayo kutokana na uzito kupita kiasi hasa majogoo pia sakafu yako sio laini (ina changarawe, mchanga mgumu au k**a umeweka sakafu ya waya/nyavu basi hazijakaa vizuri zinawachoma kuku), bembea/vichanja vipo juu zaidi ya mita 1 kutoka sakafuni na k**a umeweka matandaza kwenye sakafu basi ujue hayana kina cha kutosha.
Baada ya kusahihisha makosa, sasa kimbia nenda ukatibu ugonjwa kiurahisi kutumia binzari ya manjano.
Chakufanya, chukua kitu chenye ncha kali k**a kisu chembamba kisha kichome kwenye moto kuua vijidudu alafu tumbua huo uvimbe kwa kuku. Kamua hadi uchafu wote utoke, safisha kwa maji ya vuguvugu yenye chumvi kwa mbaali. Ili maji yaingie kusafisha vizuri hadi ndani unaweza kutumia bomba safi la sindano kuvuta maji na kusafisha ndani ulipotoa uchafu. Pakishakuwa safi weka au nyunyizia unga wa binzari na umfunge jeraha kwa kitambaa kisafi.
Zingatia: Wakati unatumbua uwe umevaa groves, lainisha miguu kwa kuiloweka kwenye maji safi yenye sabuni ya unga kwa dk 10, ifute miguu na upake sanitizer au spirit, mfunge kuku kitambaa ili atulie kisha tumbua mguu kwa kutumia kisu kwa kukata doa au baka jeusi kwanza kisha kamua kuondoa kokwa lote.
Weka dawa hii kwenye kidonda mara moja kila siku hadi kuku atakapopona. Siku 5 nyingi utaona kuku wamepona kabisa.
Binzari ya manjano ni tiba supa kwa magonjwa ya numonia ya fangasi (Aspergillosis), minyoo, kikohozi, mafua, kuharisha, ndui ya kuku, kuhara damu (coccidiosis) na magonjwa mengine yanayosababishwa na bakteria.
Kwa wale wanaopenda pesa za chapchap binzari ya manjano ni rafiki yao wa karibu kwani matumizi yake hongeza utagaji wa mayai, mayai hata ya kuku wa kisasa yanaweza kufanywa kuwa na kiini cha njano k**a vile ya kuku wa kienyeji wa shamba, hufanya kuku wakue haraka, wawe wazito na wachangamfu n.k
Nipo ninakuandalia kitabu chako ambacho Mungu akipenda mwezi wa 6 kitakuwa mkononi mwako ili ujue mambo haya kwa undani na uwe unasikia magonjwa kwa majirani tu. Ahahahahah
Kitabu kitakua na dawa zaidi ya 100 zenye kutibu karibu magonjwa yote yanayosumbua kuku wako. Pia nitakuwekea na busta kibao za chakula zitakazofanya upate mshiko fasta bila kusubirisubiri afu na bidhaa zako ziwe bora bila mshindani.
Kwa leo naishia hapa. Niambie unataka kujifunza nini zaidi? Nitakuandalia mada yako maalumu hapahapa.
Somo hili ni zawadi kwako baada ya jana Singida Poultry Farm kuleta mrejesho mzuri sana baada ya kufanyia kazi kwa mafanikio somo nililoweka siku ya ijumaa kuhusu JINSI YA KUWAPATIA KUKU CHAKULA BORA BILA GHARAMA.
Masomo mengi yatakuja baada ya kupokea mrejesho kutoka kwako jinsi unavyotumia masomo haya.
Tuvute pamoja. Pesa mfukoni, akili kichwani na Mungu moyoni.