29/01/2026
Kocha wa Zamani wa Simba SC raia wa Algeria ameendelea kugonga vichwa vya vigogo wa soka barani Afrika baada ya kuonyesha misimamo yake mikali ya maisha yake ya soka
Benchikha imekuwa ngumu kusikia amefutwa kazi kwenye klabu yyte badala yake yeye hua anaacha kazi mapema kabisa
Unakumbuka alipokua Simba SC Benchika aliacha kazi baada ya muda mchache tu alioutumia ndani ya kikosi hicho akieleza ana matatizo ya kifamilia na kutimkia JS Kabylie
Huko pia alikaa kwa muda mchache akasema hana amani, mashabiki wanatishia usalama wake na familia yake akawasilisha barua ya kuachia ngazi kwenye klabu hiyo akatimkia USM Alger
Nako amewasilisha jana barua ya kuachia ngazi, na kufanya rekodi yake ya kutodumu kwenye vilabu kuendelea
Je wapi anaelekea mwamba huyu??