31/01/2026
Ilikuwa 2019 nimetoka dar nimerudi nyumbani tabora, niliamua kurudi tabora baada ya maisha ya Dar kunishinda, Dar niliishi maisha magumu sana, hata nauli ya kurudi tabora nilimuomba mama anitumie, alifanya vibarua mwisho akawa amepata na akawa amenitumia, ilikuwa mwezi wa 12 kipindi Cha masika.
Nilivyo fika tabora nilifikia nyumbani k**a kawaida, nikaanza maisha mapya nikawa napiga vibarua sana tu mpaka nikapata mtaji laki Moja nikawa naenda kubeba magogo porini naleta mjini Ili yapasuliwe niuze mbao, nilienda safari mbili tu mali asili Waka nik**ata na kuninyanganya Kila kitu pamoja na Baiskeli, nikabaki sina pakushika tena, ikabidi nirudi kwenye vibarua tena, nikapata tena laki ikabidi nifungue genge nyumbani kwetu pale, lakini ndani ya wiki tu nikiwa nimetoka usiku kwenda kuangalia mpira nilikuta wame beba Kila kitu, ilikuwa mwezi wa pili 2020.
Baada ya hapo nilimuomba mama anipe nauli niende mgodini kahama, mama alinipa elfu 15 nikapanda gari nikaenda, nilivyo fika kahama Kuna rafiki yangu wa nyumbani kwetu akanipeleka mpaka mgodini akaniunganisha na watu wake, kesho yake asubuhi tuliingia kuchimba, kilicho tokea ni kitu Cha kusikitisha, njia tuliyo ingilia kifusi kikadondoka, tulikaa huko chini siku tatu wenzetu watatu wali fariki tukabakia wawili ndo tulio okolewa, nilipelekwa hospital na baada ya hapo nilipewa nauli nikarudi tu nyumbani.
Baada ya hapo nilikata tamaa ya maisha mpaka nikawa nawaza kujiua, niliendelea kuishi hivyo hivyo, nikipata vibarua napiga Ili nipate pesa ya kula na kusaidia pale nyumbani, nikawa siwazi tena kuhusu Biashara.
Dada sisi ukoo wetu tuna kawaida Kila inapo fikia sikukuu ya pasaka lazima watu wote tukusanyike haijarishi wewe ni muislam au mkiristo, ulisha pangwa lazima ufike, Sasa bwana ndugu wote walikuja kutoka mikoa mbalimbali, kawaida huwa tunakaa wiki tukijadiliana baadhi ya mambo pia tuna kula na kunywa.
Baada ya sikukuu ya pasaka zilipita siku tatu, mtoto wa baba yetu mkubwa akapata ajali, aliangukiwa na mti akavunjika uti wa mgongo, Sasa ikabidi Wana ukoo wote tuitwe pale Ili tuchangie pesa ikodiwe gari apelekwe muhimbili, watu wote walianza kuchangia pesa, wengine mpaka wadogo zangu wanatoa pesa nyingi pale kwenye beseni halafu mimi sina hata mia, siku hiyo niliona aibu mpaka nikahisi ni siku mbaya maishani mwangu.
Baada ya hapo nilipata uchungu sana, nikaamua ngoja tu nikajiue sina thamani yoyote, nilienda kimya kimya kwenye pori ambalo liko mbali kidogo kutoka nyumbani, niliwaambia naenda kuchuma (miduguyu), Kwa watu wa tabora Wana elewa haya matunda.
Nilivyo fika porini nilikaa chini nikaanza kulia nalalamika kwanini Mimi yani, Kila ninacho fanya hakiendi, nililia sana huku nimekaa na badae uchungu ulizidi nikalala chali huku naendelea kulia, Badae nilinyamaza huku nimelala chali hivyo hivyo, nikawaza bora tu nijiue Sina maana yoyote ya kuishi na Sina chakupoteza Duniani, ikabidi niinuke, Ile tu nainuka Ghafla nikamuona marehemu bibi yangu mbele yangu, nilish*tuka sana nikataka kukimbia, nilivyo jaribu kukimbia tu miguu ikawa k**a imenasa kwenye Ardhi Yani mguu nikinyanyua hautoki chini, Bibi akawa ananitazama tu, mara akanisogelea huku mkononi kashika noti ya elfu 10, nikawa Kila nikijaribu kupiga kelele sauti inatoka kweli ila watu ambao nilikuwa nawaona mashambani kwao wakawa hawanisikii wakati siyo mbali sana, ila mwisho bibi alinipa mkononi Ile elfu 10 akaniambia hiyo hela kaweke juu ya kaburi langu, Baada ya hapo bibi alitembea kinyume nyume hatua 4 akawa amepotea ghafla, hapo na Mimi nikawa nimekimbia kurudi nyu