05/07/2026
Mh. Mohamed Laki, Mbunge wa Jimbo la Kwahani, alihudhuria mechi ya Kombe la Yamle Yamle Cup iliyowakutanisha Kwahani dhidi ya Mwene Combine. Timu ya Kwahani iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4–1. Uwepo wa Mh. Mbunge katika mechi hiyo umeonyesha mshik**ano, hamasa na sapoti yake kwa vijana, pamoja na kuendelea kuhimiza ushiriki wao katika michezo k**a njia ya kukuza vipaji, kuimarisha afya na kuendeleza umoja wa jamii.
Aidha, Mh. Mohamed Laki aliwapongeza waandaaji na wasimamizi wa Yamle Yamle Cup kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuandaa mashindano hayo kwa weledi na mafanikio. Aliwashukuru kwa kuanzisha na kuendeleza mpango wenye maono mapana unaochangia kukuza vipaji vya vijana, kuimarisha mshik**ano wa jamii na kuitangaza Zanzibar pamoja na Tanzania kwa ujumla kupitia michezo. Alisisitiza kuwa jitihada k**a hizi zinastahili kuungwa mkono na wadau wote kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.