26/04/2026
DIAMOND MAPAFU YA MBWA – AIMBA MASAA 8 BILA KUSHUKA JUKWAANI
Show ya msanii mkubwa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, kupitia ziara yake ya Retro Tour imeanza kwa kishindo kikubwa huku akivunja rekodi ya aina yake jijini Mwanza. Katika tukio hilo lililovuta maelfu ya mashabiki, Diamond ameweka historia mpya kwa kupanda jukwaani na kuimba kwa takribani masaa nane mfululizo bila kushuka, akitoa burudani mpaka alfajiri ambapo jua lilianza kuchomoza.
Kuanzia alipokanyaga jukwaani, Diamond hakupumzika hata kidogo. Alianza na nyimbo zake za zamani zilizompa umaarufu mkubwa k**a Nenda Kamwambie, na kuendelea kuwapa mashabiki burudani kwa hit song zake zote mpaka zile mpya k**a Ikweji (Joy). Ilikuwa ni safari ya muziki iliyoonyesha ukuaji wake kisanii na uwezo wake mkubwa wa kutawala jukwaa kwa muda mrefu bila kuchoka.
Katika show hiyo, Diamond alionyesha kwa vitendo kwanini anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii bora Afrika linapokuja suala la live performance. Sauti yake ilikuwa thabiti, nguvu zake jukwaani hazikupungua, na mawasiliano yake na mashabiki yalikuwa ya kiwango cha juu kabisa. Kila wimbo uliimbwa uliambatana na nishati kubwa, dansi kali, na msisimko uliowafanya mashabiki kushindwa kukaa chini.
Si Diamond pekee aliyeonyesha uwezo wa kipekee, bali pia mashabiki wake walionyesha mapenzi na uvumilivu wa hali ya juu. Licha ya show kudumu kwa muda mrefu usiku kucha, mashabiki hawakuondoka wala kuchoka. Waliendelea kuimba pamoja naye, kurukaruka na kushangilia kila wimbo, kana kwamba muda haukuwapo. Ndipo ikazaliwa kauli maarufu ya usiku huo kuwa, “Diamond ana mapafu ya mbwa, na mashabiki wana mapafu ya samaki.”
Tukio hilo halikuwa tu show ya kawaida, bali liligeuka kuwa historia na kumbukumbu isiyofutika kwa wakazi wa Mwanza na wadau wa muziki kwa ujumla. Ilikuwa zaidi ya burudani – ilikuwa ni tamasha lililoonyesha nguvu ya muziki, mshik**ano wa msanii na mashabiki wake, pamoja na kiwango cha juu cha juhudi na kujituma kwa Diamond Platnumz.
Kwa hakika, uzinduzi wa Retro Tour umeweka kiwango kipya na matarajio makubwa kwa miji mingine itakayofuata. K**a Mwanza imeanza hivi, basi mashabiki wanapaswa kujiandaa kwa maajabu zaidi kutoka kwa msanii huyu ambaye ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni mfalme wa jukwaa.