26/12/2025
Kabla ya mwaka huu wa 2025 kuisha, hakuna ubaya ukafahamu kuhusu aina na tabia ya asali katika mazingira ya mahitaji yako.
KITABIA, ASALI YA NYUKI WAKUBWA IKO HIVI;
1. Haina uchachu hata kidogo k**a ilivyo asali ya nyuki wadogo, mara nyingi huwa tamu moja kwa moja.
2. Asali ya nyuki wa aina hii hutofautiana rangi, wakati mwingine inaweza kuwa nyeupe, njano, kahawia na kadhalika. Hii hutokea kutegemeana na malisho ya nyuki (foraging).
3. Ina kiwango cha maji kuanzia 17% na hakizidi 20%, kwa hiyo ni nzito sio nyepesi k**a ile ya nyuki wadogo.
Wakati,
ASALI YA NYUKI WADOGO IKO HIVI;
1. Inaharufu kali kidogo.
2. Ina rangi ya kahawia, mara nyingi kahawia iliyokolea inayoenda kwenye weusi.
3. Huwa nyepesi sana kwani ina kiwango cha maji kinachoanzia 24%.
4. Ni tamu sana but ina ladha ya uchachu kwa mbali kadri ya muda tangu ivunwe.
Kwa mwenye uhitaji kwenye sikukuu hizi, shika simu yako na piga +255759886429. Unaletewa kokote isipokuwa kuzimu, utani.
Karibuni Shamba la Nyuki Biharamulo.