FumboX

FumboX FumboX ni nyumbani kwa hadithi za maisha halisi—za kusikitisha, kusisimua na zenye mafunzo. Jiunge nasi kugundua ukweli uliofichwa nyuma ya maisha ya kila siku.

17/05/2026

MKE WA MCHUNGAJI, mama wa siku inapatikana katika youtube channel yetu

17/05/2026

HOUSEGIRL WA USIKU....SEHEMU YA 3 — Siri ya Nyumba ya MwishoKaribu kwenye sehemu ya tatu…ya Housegirl wa Usiku…Asha alip...
08/05/2026

HOUSEGIRL WA USIKU....
SEHEMU YA 3 — Siri ya Nyumba ya Mwisho

Karibu kwenye sehemu ya tatu…
ya Housegirl wa Usiku…

Asha alipiga kelele kubwa.
“AAAAAHHH!”
Mtu yule mrefu aliyekuwa kona ya chumba…
alitoweka ghafla…
k**a moshi mweusi.

TAA!
Umeme ukarudi sekunde hiyo hiyo.
Rehema alikuwa amekaa peke yake sakafuni…
kana kwamba hakuna kilichotokea.
“Asha?” Bw. Musa aliita huku akikimbia kuelekea chumbani.
“Kuna nini?”
Asha alikuwa anatetemeka vibaya.
“Ndani ya hiki chumba…”
“kulikuwa na mtu!”
Bw. Musa aliangaza kila kona.
Lakini…
hakukuwa na kitu.
Rehema waliinua macho yake polepole.
“Mama ameota vibaya…”

“USIDANGANYE!” Asha alipaza sauti.
“Nimeona mtu humu ndani!”
Lakini Rehema…
hakujibu.
Alitabasamu tu.

Na hapo ndipo Bw. Musa alianza kuona kitu cha ajabu.
Miguu ya Rehema…
ilikuwa imejaa matope meusi.
Kana kwamba…
ametoka kaburini.

Asubuhi iliyofuata…
Asha aliamua kwenda kwa Bi. Komba kutafuta ukweli.
Nyumba ya mzee huyo…
ilikuwa mwisho wa mtaa.
Karibu na nyumba iliyotelekezwa iliyofunikwa na miti.
Bi. Komba alipowaona…
aliwafungia mlango haraka.
“Mlikuwa mnaambiwa msimkaribishe huyo msichana!”
“Tuambie ukweli…”
Asha alisema kwa sauti ya kuomba.
“Rehema ni nani?”

Mzee huyo alikaa kimya kwa muda.
Kisha akaanza kusema taratibu.
“Miaka mitatu iliyopita…”
“familia moja iliishi kwenye ile nyumba ya mwisho…”
Aliinua kidole kuelekea nyumba iliyotelekezwa.
“Walikuwa na housegirl anaitwa Rehema…”

Bw. Musa akameza mate.
“Siku moja mtoto wao mdogo alipotea usiku…”
“Hakupatikana?”
Bi. Komba akatikisa kichwa.
“Baada ya siku tatu…”
“wakampata chini ya kitanda chake…”
“amekufa.”

Asha alihisi mwili ukimtetemeka.
“Na Rehema?”
“Mwenye nyumba alimlaumu Rehema…”
“Wakasema alikuwa mchawi.”
“Nini kilitokea?”
“Wananchi walimfukuza usiku wa mvua…”
“Siku iliyofuata…”
“walimkuta amekufa karibu na kisima cha nyuma ya nyumba.”

“Mwisho wa mazishi yake…”
“watu walianza kusikia sauti usiku.”
“Sauti gani?”

“Narudi kuchukua aliyebaki…”

Usiku ulipoingia tena…
Neema alianza kuumwa ghafla.
Mwili wake ulikuwa wa moto sana.
Lakini kila alipofumba macho…
alikuwa anarudia maneno yale yale.
“Yuko chini ya kitanda…”
“Ananiita…”

Bw. Musa akaamua.
“Huyu Rehema lazima aondoke leo.”
Wakamtafuta nyumba nzima.
Hakuwapo.
Lakini mlango wa nyuma ulikuwa wazi.
Na matope meusi…
yalionekana kuelekea ile nyumba iliyotelekezwa.
Mvua ilianza tena walipofika mbele ya nyumba hiyo.
Mlango wake ulikuwa umefunguka wenyewe.
Kreeeeek…

Harufu ya kuoza ilitoka ndani.
Bw. Musa aliangaza tochi.
Ukutani kulikuwa na michoro ya ajabu kwa damu iliyokauka.
Na katikati ya sebule…
kulikuwa na picha ya zamani ya familia iliyokuwa ikiishi hapo.
Asha aliikaribia taratibu.
Kisha macho yake yakapanuka kwa hofu.
Kwenye picha hiyo…

Rehema alikuwa amesimama nyuma ya mtoto mdogo.
Lakini uso wake…
haukuwa wa kawaida.
Macho yake yote yalikuwa meusi kabisa.
Na nyuma ya picha hiyo…
kulikuwa na maneno yaliyoandikwa kwa damu.
“MTOTO WA MWISHO BADO YUPO.”

Inaendelea Sehemu ya 4......


PENZI LA HOSPITALINISEHEMU YA 1Mvua nzito ilifunika anga la jiji la Dar es Salaam usiku ule. Radi zilikuwa zikigonga mad...
08/05/2026

PENZI LA HOSPITALINI
SEHEMU YA 1
Mvua nzito ilifunika anga la jiji la Dar es Salaam usiku ule. Radi zilikuwa zikigonga madirisha ya hospitali ya kisasa ya MediCare International, huku wagonjwa wachache wakikimbizwa kwenye vyumba vya dharura.

Ndani ya hospitali hiyo, Daktari Careen Katunzi alikuwa bado kazini licha ya kuwa muda wake wa zamu ulikuwa umeisha saa moja iliyopita.
“Doctor Careen, unaweza kwenda kupumzika sasa,” muuguzi mmoja alimwambia.
Careen akatikisa kichwa.
“Nitamaliza faili hizi kwanza.”

Kila mtu hospitalini alimjua Careen k**a mwanamke mwenye moyo wa kazi lakini asiyechangamana sana. Hakupenda stori za mapenzi wala mahusiano. Wengi walidhani alikuwa na kiburi, lakini ukweli ni kwamba moyo wake uliwahi kuvunjwa vibaya miaka iliyopita.
Akiwa bado amekaa ofisini, ghafla kelele zilisikika koridoni.

“Emergency! Emergency!”
Madaktari na wauguzi wakaanza kukimbia.
Careen akasimama haraka.
Mlangoni waliingia na machela iliyombeba mwanaume aliyekuwa amepoteza fahamu. Uso wake ulikuwa umejaa damu kidogo huku mkono wake wa kushoto ukiwa umejeruhiwa vibaya.
“Ajali ya gari,” mmoja wa wahudumu alisema kwa haraka.
Careen akamsogelea.
“Mapigo ya moyo?”
“Yapo lakini dhaifu.”
“Tumpeleke theatre sasa!”

Dakika kadhaa baadaye, Careen alikuwa akifanya kila alichoweza kuokoa maisha ya mwanaume huyo asiyejulikana.
Baada ya muda mrefu wa presha, hatimaye hali yake ikatulia.
Careen akavuta pumzi ndefu.
“Tumemuokoa.”
Alipogeuka kuondoka, ghafla mkono wa yule kijana ukamshika.
Macho yake yakafumbuka polepole.
Na kwa sauti dhaifu sana akasema:
“Usiondoke…”
Careen aliganda.

Kulikuwa na kitu kwenye macho yale kilichomfanya ashindwe kuondoka mara moja.
Lakini kabla hajauliza chochote, kijana huyo akapoteza fahamu tena.

Asubuhi iliyofuata, Careen alirudi hospitalini mapema kuliko kawaida.
Hakuelewa ni kwa nini alikuwa akifikiria sana kuhusu mgonjwa yule.
Alifika kwenye chumba chake.
Kijana huyo alikuwa macho sasa, akitazama dirishani kimya.
“Habari yako leo?” Careen aliuliza.
Kijana akamwangalia.
Kwa mara ya kwanza, Careen aliuona vizuri uso wake.

Alikuwa handsome kupita kawaida… lakini macho yake yalikuwa na huzuni nzito sana.
“Uko hospitalini salama,” Careen alisema.
“Jina lako nani?”
Kijana akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kujibu:
“Ryan.”
“Ryan nani?”
“Ryan Mbeki.”
Ryan Mbeki aliongea kwa sauti tulivu lakini yenye uchovu mkubwa.
“Una ndugu tukuwasiliane nao?”
Ryan akageuza uso pembeni.
“Hakuna.”
Jibu lile lilimfanya Careen ashangae.
“Mtu yeyote? Rafiki?”
Ryan akatikisa kichwa polepole.
“Sitaki mtu ajue niko hapa.”
Kulikuwa na siri nzito nyuma ya maneno yale.
Careen akaamua kutomsumbua.
Lakini kabla hajaondoka, Ryan akamuita tena.
“Doctor…”
“Hmm?”
“Asante kwa kuniokoa.”
Careen akatabasamu kidogo.
Lilikuwa tabasamu lake la kwanza la kweli kwa muda mrefu sana.

Usiku huo, Careen alipokuwa anarudi nyumbani, hakuweza kuacha kumfikiria Ryan.
Kulikuwa na jambo lisiloeleweka kuhusu mwanaume huyo.
Ajali yake.
Upweke wake.
Na huzuni iliyokuwa machoni mwake.
Hakujua kwamba huo ulikuwa mwanzo wa hadithi ambayo ingebadilisha maisha yake yote.

Inaendelea.......sehemu ya 2

HOUSEGIRL  WA USIKUPart 2:Usiku ulipoingia tena, hali ndani ya nyumba ya Bw. Musa ilibadilika kabisa.Hakuna aliyekuwa ak...
07/05/2026

HOUSEGIRL WA USIKU
Part 2:
Usiku ulipoingia tena, hali ndani ya nyumba ya Bw. Musa ilibadilika kabisa.
Hakuna aliyekuwa akizungumza sana mezani.
Maneno ya Bi. Komba yalikuwa bado yanamzunguka Asha kichwani:
“Housegirl huyo alikufa miaka mitatu iliyopita…”
Asha alijaribu kujipa moyo.
“Labda ni mtu mwingine tu anayefanana naye,” alijiambia.
Lakini Neema hakutaka hata kukaa karibu na Rehema.
Kila Rehema alipopita, mtoto huyo alijificha nyuma ya mama yake.
“Mama… huyo dada huwa hapepesi macho,” Neema alinong’ona.
Asha alitabasamu kwa kulazimisha.
“Usiogope mwanangu.”
Lakini moyoni… hata yeye alianza kuogopa.
Usiku wa manane ulipofika, umeme ulikatika ghafla.

Nyumba nzima ikaingia gizani.
Mvua ilianza kunyesha tena nje huku upepo ukigonga madirisha.
Bw. Musa aliwasha tochi.
“Hii TANESCO bana…” alisema huku akielekea sebuleni.
Lakini kabla hajafika mbali…
alisikia hatua nzito kutoka juu ya dari.
Guu… guu… guu…
Akasimama.
“Asha… kuna mtu juu?”
“Hakuna.”
Hatua zile ziliendelea polepole kana kwamba mtu alikuwa anatembea juu ya paa.
Neema akaanza kulia chumbani.
“MAMAAAA!!”
Asha alikimbia haraka.
Walipofika chumbani kwa Neema, walimkuta amejifunika blanketi lote huku akitetemeka.
“Kuna nini?” Bw. Musa aliuliza.
Neema alinyanyua kidole chake taratibu kuelekea chini ya kitanda.
“Kuna mtu anaongea…”
Wote wakakaa kimya.
Na kweli…
chini ya kitanda kulisikika sauti ya mwanamke ikinong’ona:
“Neema… njoo huku chini…”
Asha alipiga kelele.
Bw. Musa akainama haraka na kuangaza tochi chini ya kitanda.
Hakukuwa na mtu.
Lakini…
kulikuwa na matope mapya sakafuni. Na harufu kali ya udongo wa makaburini ilijaa chumbani.
Dakika chache baadaye, walimsikia Rehema akiimba taratibu jikoni.
Sauti yake ilikuwa ya ajabu… nzito… k**a mtu anayelia.
Asha akaenda jikoni kwa hasira.
“Rehema! Ulikuwa chumbani kwa mtoto?”
Rehema aligeuka polepole.
Mikono yake ilikuwa imelowa maji meusi.
“Hapana mama.”
“Kwa nini mikono yako iko hivyo?”
Rehema alitazama mikono yake kana kwamba hakuona chochote.
“Kuna nini?”
Asha alirudi nyuma kwa hofu.
Ghafla Neema alitokea mlangoni akiwa analia.
“Mama… huyo dada si binadamu…”
Rehema akainama kidogo na kumwangalia Neema moja kwa moja machoni.
Kisha kwa sauti ya chini sana akasema:
“Aliniita nirudi…”
“Kina nani?” Asha aliuliza kwa sauti ya kutetemeka.
Rehema hakujibu.
Badala yake… aligeuza kichwa chake taratibu kuelekea ukutani.
Kana kwamba alikuwa anamsikiliza mtu mwingine.
Usiku huo, Asha hakulala.
Majira ya saa tisa za usiku, aliamka kwenda kunywa maji.
Alipopita karibu na chumba cha Rehema… mlango ulikuwa wazi kidogo.
Ndani kulikuwa giza tupu.
Lakini Asha alisikia sauti za watu wawili wakiongea.
Sauti ya kwanza ilikuwa ya Rehema.
Sauti ya pili… ilikuwa nzito sana… si ya kawaida.
“Bado hawajajua ukweli…”
“Mtoto ndiye aliyebaki…”
Asha akahisi damu ikimganda.
Alisukuma mlango taratibu…
Na alichokiona kilimfanya ashindwe kupumua.
Rehema alikuwa amekaa sakafuni.
Lakini hakuwa peke yake.
Kwenye kona ya chumba…
kulikuwa na mtu mrefu mweusi kabisa aliyesimama ukutani.
Macho yake yalikuwa meupe yanang’aa gizani.
Na kichwa chake…
kilikuwa kimegeuka nyuma kabisa.

Inaendelea........Part 3 Usikose...Follow page yetu kuendelea kusoma hadithi zetu nzuri


HOUSEGIRL WA USIKU.Part 1:Sitamsahau Mgeni wa Ajabu aliyekuja nyumbani usiku ule.........Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha us...
07/05/2026

HOUSEGIRL WA USIKU.

Part 1:Sitamsahau Mgeni wa Ajabu aliyekuja nyumbani usiku ule.........

Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha usiku ule mjini Dar es Salaam. Radi zilipasua anga huku upepo ukitikisa madirisha ya nyumba ya familia ya Bw. Musa.
Ndani ya sebule, Asha alikuwa amekaa akimtuliza mtoto wake mdogo, Neema, aliyekuwa akilia bila sababu.
“Mama… kuna mtu dirishani…” Neema alisema kwa sauti ya chini huku akitetemeka.
Asha aligeuka haraka kuangalia dirisha. Hakukuwa na mtu.
“Unaota tu mwanangu,” alisema huku akimfunika blanketi.
Lakini kabla hajamaliza kusema, mlango wa mbele ulisikika ukigongwa taratibu…
GONG… GONG… GONG…
Bw. Musa alitoka chumbani akiwa amechoka.
“Usiku huu nani tena?” aliuliza kwa hasira.
Alipofungua mlango, alimkuta mwanamke mwembamba aliyelowa maji kabisa. Alikuwa amevaa gauni jeusi refu, macho yake yalionekana kuchoka sana.
“Samaḥani… naitwa Rehema,” alisema kwa sauti ya upole.
“Natafuta kazi ya housegirl… nilipewa hii address.”
Asha alishangaa.
“Hii muda wote huu?”
Rehema aliinamisha kichwa polepole.
“Sina sehemu ya kwenda.”
Neema aliyekuwa nyuma ya mama yake alianza kulia ghafla.
“ONDOKA!” alipiga kelele.
“Yule dada ana damu mikononi!”
Wazazi wake walibaki wamemshangaa.
Lakini walipoangalia mikono ya Rehema… ilikuwa safi kabisa.
Bw. Musa akacheka kidogo.
“Mtoto ana mawazo mengi.”
Kwa sababu ya huruma, waliamua kumpa kazi na sehemu ya kulala.
Usiku huo, kila kitu kilionekana kawaida…
Mpaka saa sita usiku.
Asha aliamshwa na sauti ya vyombo jikoni.
Kling… Klang…
Alitazama saa.
12:03 AM
Aliinuka taratibu na kutoka chumbani.
Sebule ilikuwa giza. Pazia zilikuwa zikicheza kwa upepo. Lakini alipofika karibu na jikoni… alimsikia mtu akiongea kwa sauti ya chini.
Ilikuwa ni sauti ya Rehema.
“…Nimefika… ndiyo… bado hawajajua…”
Asha alishtuka.
“Rehema?” aliita.
Kimya.
Alipoingia jikoni, alimkuta Rehema amesimama peke yake gizani, akitazama ukutani.
“Mama samahani,” alisema taratibu.
“Nilikuwa nakunywa maji.”
Asha alitazama kila kona.
“Hukuwa unaongea na mtu?”
Rehema hakujibu mara moja.
Taratiiibu… akatabasamu.
“Hapana mama.”
Lakini nyuma ya Rehema, kwenye dirisha la jikoni… Asha aliona kivuli cha mtu mrefu mwenye macho meupe kikitoweka gizani.
Asubuhi iliyofuata, jirani yao mzee Bi. Komba alikuja nyumbani.
Alipomuona Rehema akifagia nje, uso wake ulibadilika ghafla.
“HAPANA…” alisema kwa sauti ya hofu.
Asha alishtuka.
“Kuna nini mama?”
Mzee huyo alianza kutetemeka.
“Msichana huyo… haiwezekani…”
“Kwa nini?”
Bi. Komba alimwangalia Rehema kwa macho yaliyojaa hofu.
“Miaka mitatu iliyopita… housegirl mwenye sura hiyo alikufa kwenye nyumba ya mwisho wa mtaa huu…”
Radi ilipiga ghafla.
Na Rehema aliyekuwa nje… alisimama kufagia.
Polepole akageuza shingo yake kuelekea dirishani.
Kisha… akatabasamu.

Inaendelea .......Part 2..Usikose



Kijiji KisichoonekanaUsiku ulianza kuingia wakati Musa alikuwa anarudi nyumbani akitokea safari ya kikazi.Gari lake lili...
06/05/2026

Kijiji Kisichoonekana

Usiku ulianza kuingia wakati Musa alikuwa anarudi nyumbani akitokea safari ya kikazi.
Gari lake lilianza kupata matatizo katikati ya msitu.
Hakukuwa na network.
Hakuna taa.
Hakuna watu.
Alipojaribu kutafuta msaada kwa miguu…
Aliona taa kwa mbali.
Alipokaribia… aligundua ni kijiji.
Lakini cha ajabu—hakukuwa na sauti ya watoto.
Hakuna mbwa.
Hakuna hata upepo.
Watu waliokuwa pale walimkaribisha kwa tabasamu… lakini macho yao yalionekana tupu.

Musa alipewa chakula na mahali pa kulala.
Lakini alihisi kuna kitu si cha kawaida.
Alipotoka nje kidogo usiku…
Aliwaona watu wakitembea kimya kimya.
Ndipo alipogundua kitu cha kutisha—
Hakuna hata mmoja wao alikuwa na kivuli.
Moyo wake ulianza kudunda.
Alipojaribu kurudi ndani…
Mlango ulikuwa umefungwa kutoka nje.

Asubuhi ilipofika, Musa aliwauliza kuhusu njia ya kutoka.
Mzee mmoja alimwambia kwa sauti ya baridi:
“Hapa hakuna anayeondoka bila ruhusa.”
Musa alichukua simu yake kuangalia ramani…
Kijiji hakikuonekana kabisa.
Na ghafla akapokea message isiyojulikana:
“Uliingia… sasa ni zamu yako kubaki.”
Alipoangalia juu… watu wote walikuwa wanamtazama kimya kimya.

Musa alianza kuchunguza kwa siri.
Aligundua nyumba moja iliyofungwa.
Alipoingia… alikuta picha nyingi za watu.
Watu waliopotea miaka tofauti.
Wote walikuwa wageni waliowahi kufika hapo.
Na kwenye ukuta wa mwisho…
Kulikuwa na nafasi tupu—na chini yake jina lake tayari limeandikwa:
“MUSA”
Ghafla mlango ulijifunga kwa nguvu.

Usiku ulipoingia… watu wote walikusanyika katikati ya kijiji.
Mzee yule alisimama mbele yake:
“Kila baada ya miaka kadhaa… kijiji kinahitaji mtu mpya.”
Ardhi ilianza kutetemeka.
Kivuli chake… kilianza kupotea polepole.
Musa alipiga kelele, akijaribu kukimbia…
Lakini miguu yake haikusogea.
Kesho yake…
Barabara ile ile ilionekana tena.
Wasafiri wengine walipita.
Na mbali kidogo… waliona kijiji.
Mmoja wao akasema:
“Twendeni pale kuomba msaada…”
Na Musa…
Alikuwa amesimama pale kijijini, akitabasamu kimya—
Bila kivuli.

MWISHO.



05/05/2026

Hakuna kofia hakuna nafasi yapili...

Address

Kimara, Dar Es Salam
Dar Es Salaam
16104

Opening Hours

Monday 07:00 - 17:00
Tuesday 07:00 - 17:00
Wednesday 07:00 - 17:00
Thursday 07:00 - 17:00
Friday 07:00 - 17:00
Saturday 07:00 - 17:00
Sunday 07:00 - 17:00

Telephone

+255753438466

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FumboX posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to FumboX:

Shortcuts

Share