05/01/2024
UKWELI WA MAMBO..
Ingawa kwa jamii zetu asilimia kubwa mkulima anaonekana kudharauliwa k**a mtu aliyekosa kazi ya Kufanya kujiingizia kipato, Lakini ukweli ni kwamba Kazi ambayo alipewa mwanadamu au mtu wa kwanza ni Kulima, (Kutunza Bustani).
Na katika hili, Baraka nyingi sana zimeamliwa na Muumbaji.
Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu mwenye uhai anamhitaji mkulima ili aendelee kuishi katika afya njema..
Kwa wale wanaotumia neno serikali imesahau, Basi moja ya mtendaji mwaminifu aliyesahaulika kwa swala la masilahi ni mkulima,. Kauli hii ni dhahili kwa wale wakulima wenye uwezo mdogo, maana ufanyia kazi tumbo na wakati mwingine isitoshe.. Kwa wale wenye mitaji mkubwa ndio wenye ujasili wa kusimama na kusema hakuna kazi yenye faida k**a Kilimo.
Naam, ni Ukweli Usiopingika kuwa kilimo ni ajira tamu sana , ni kazi yenye faida kubwa kwa mtu aliyedhamilia kulima kibiashara,..
Kilimo hakitaki papala, maana ni kazi inayoendeshwa na maarifa ya Kisayansi, mazoea na kuiga imewafanya wengi wanakichukia Kilimo kwa maarifa maarufu k**a ujuaji na mwisho wa siku wameanbulia patupu..
Mpangilio wa Lishe uanzia shambani, mababu zetu waliishi miaka mingi ya nguvu za mwili kwa vyakula walivyokula wakati huo, vyakula visivyochakachuliwa, yaana vyakula vya asili. Ni Ukweli Usiopingika Leo ukisasa na ubunifu umeleta vyakula laini na visivyomuandaa mtu kuishi miaka mingi yenye afya njema..
Back to Eden Asili Yetu imedhamilia kutoa huduma ya kueneza Elimu juu ya Kilimo na Umuhimu wa kula Chakula bora kwa usitawi wa Kizazi Cha sasa na kijacho...
Twende Pamoja bila kusahau Mbegu bora kutoka EPINAV AGRICULTURAL SOLUTIONS..
Nyanya
Captain F1
BANSAL F1
SALINA F1
Tanzanite F1
Hoho
Supreme F1
Gambia F1
Cabbage
Tunu F1
Vitunguu
Red Planet F1
Tikiti maji
Jumbo F1
Bila kusahau mbolea za maji, ambazo soon zitakuwa sokoni kwa manufaa ya mkulima wa Kitanzania..
Weka order yako popote ulipo ujipatie bidhaa bora kwa shamba lako....