25/08/2026
Makosa matano ya kuepuka ukiwa unalisha kuku wako
1. Uwekaji wa chakula, inabidi ujue ni kiasi gani cha chakula uweke.
Usiweke tuu chakula kwa kuhisi hiki kingi au kinatosha, jitahidi ujue kiasi gani kuku wako wanahitaji na inabidi ujue ni kiasi gani wanakula kwa siku.
Chakula kidogo sana hakikuzi kuku na kingi sana kina ongeza upotezefu wa chakula.👌🏼
2. Kujaza chakula kwenye malishio hadi juu (ukomo)
Hii nayo inapoteza chakula kirahisi sana, feeder ikijaa kupita kiasi kuku wanaparua na kumwaga chakula sana, weka ujazo unaotakiwa sio hadi juu kabisa👌🏼
3. Ubadilisha chakula gafla;
Kwa kawaida tunasema 75/25 alafu 50/50 alafu 25/75 kila inapotakiwa kuwapa chakula tafauti, mf; kutoka starter kwenda grower, kuku wanahitaji kuzoea chakula kipya taratibu, kubadilisha gafla kunaleta stress kwa kuku hivyo ukuaji hubadilika.👌🏼
4. Kuacha chombo cha chakula kibichi au kikiwa kichafu;
Maji yakimwagikia kwenye chakula hata kidogo tuu ni kheri kutoa chakula kuliko kuona uvivu na kuacha kutoa, ni chanzo kikubwa cha magonjwa kwa kuku, jitahidi kutoa chakula kilichogusana na maji.👌🏼
5. Kutokuacha nafasi nzuri ya vyombo vya chakula;( spacing)
Unaweza kua na vyombo vya kutosha na bado kuku hawashibi, broila wavivu vyombo inabidi vipqngwe vizuri,
Kuku wenye nguvu watakula zaidi wakati wale walegevu hawatashiba, jitahidi kuwatenga kuku wale wakubwa na wadogo ila nao wapate chakula na wakue vizuri.👌🏼
Kumbuka kukuza kuku sio tu chakula cha gharama au kizuri ni kuhusu,
😊JINSI UNAVYOKIPIMA KWA KUKU😳
😊KAMA JE KUKU WOTE WANAPATA,
😊JINSI UNAVYOWAWEKEA.
Hapa ndo sisi wafugaji wengi tunapoteza pesa na kulalamika ufugaji mgumu
🤣☎️☎️0752-396249