Madam NeymaMhando

Madam NeymaMhando Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Madam NeymaMhando, Grocers, Tanga.

23/05/2026
HUENDA HATA WEWE UNAMFUGA NYOKA MKUBWA SANA BILA KUJUA...NI Kisa cha Nyoka mwenye njaa na mwanamke mwema ni kisa cha mfa...
06/02/2026

HUENDA HATA WEWE UNAMFUGA NYOKA MKUBWA SANA BILA KUJUA...

NI Kisa cha Nyoka mwenye njaa na mwanamke mwema ni kisa cha mfano,
Kisa kinachotuonya juu ya watu wanaotuzunguka kwa sura ya urafiki,
lakini ndani ya mioyo yao wamejificha k**a maadui tena wakubwa...

Ni kisa kinachotukumbusha kuwa si kila anayekukaribia anakupenda,
wapo wanaosubiri muda mwafaka ili wakumeze au wakumalize....

Inasimuliwa kuwa…

Siku moja, mwanamke mmoja mwema alimkuta nyoka mkubwa,akiwa na njaa kali na baridi kali,mwili wake ukiwa dhaifu na hauna nguvu...

Moyo wake ukamjaa huruma…
Akaamua kumuonea huruma yule nyoka.

Akamchukua, akampeleka nyumbani kwake,
akamuhifadhi, akampa makazi,akaanza kumlisha siku baada ya siku.

Muda ukapita…
Nyoka akakua mkubwa, akaanza kumzoea mwanamke yule...

Alikuwa akilala karibu naye,akimfuata kila mahali alipokwenda,kana kwamba ni rafiki wa kweli.

Lakini siku moja…
nyoka akaacha kula kabisa.

Mwanamke akahuzunika sana. akawa anamlisha kwa bidii,anamletea chakula kizuri,
lakini nyoka hakula hata chembe.

Wiki zikapita…
nyoka bado hakuli,
lakini bado anamfuata,
bado analala karibu naye,
bado anajizungusha mwilini mwake usiku akitaka joto.....

Mwanamke akafikiria sana akasema:
“Hakika nyoka wangu ni mgonjwa.”

Akaamua kumpeleka kwa daktari wa wanyama.

Daktari alipomuona nyoka, nyoka akijizungusha karibu na mwanamke huyo,
akamuliza:
“Je, ana dalili nyingine zaidi ya kukosa hamu ya kula?”

Mwanamke akasema:
“Hapana.Lakini bado analala karibu nami,hunifuatilia kwa macho,hujizungusha juu yangu usiku,lakini hataki kula kabisa.”

Daktari akatabasamu kwa huzuni…
kisha akasema kwa sauti nzito:

“Bint yangu, nyoka huyu si mgonjwa…
Anajiandaa kukula wewe.

Ameacha kula kwa makusudi
ili awe na nafasi tumboni mwake.
Anapojizungusha mwilini mwako usiku,
hapimi upendo…
anapima ukubwa wako
ili ajue k**a anaweza kukumeza.”

Maneno yale yakampiga mwanamke k**a radi.

Daktari akaendelea kusema kuwa: “Nyoka huyu Anakusanya nguvu,
anasubiri muda mwafaka wa kukushambulia.
Chukua tahadhari…
na ujitenge naye mara moja.”

Naam inaisha namna hiyo, ni hadithi ya kutisha…lakini ujumbe wake ni wa kweli sana.

Kila siku,
kuna watu wanaokaribia maisha yetu kwa tabasamu, kwa maneno matamu, kwa sura ya upole…

Lakini ndani yao,
wameficha chuki, wivu na nia mbaya na hao ndo wanatufanyia mambo ya hovyo mpaka mambo yetu yanakuwa magumu.

Sio kila mtu anaweza kubadilishwa kwa upendo.Sio kila roho ina tiba ya huruma.



*️⃣NYIRADI ZA ASUBUHI⏱️Muda :Baada ya kuchomoza kwa alfajir(Fajr) hadi kabla ya jua kuchomoza.1. Read Ayatul Kursiأَعُوذ...
01/02/2026

*️⃣NYIRADI ZA ASUBUHI

⏱️Muda :Baada ya kuchomoza kwa alfajir(Fajr) hadi kabla ya jua kuchomoza.

1. Read Ayatul Kursi

أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ، لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ، لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ، مَنْ ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ، يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ، وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاءَ، وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ، وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا، وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

"Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyumu. laa ta'khudhuhuu sinatuw wa laa nauum. lahuu maa fissamaawaati wa maa fil ardhi. man dhal ladhii yashfa'u'indahuu illaa bi idhnihi. ya'lamu maa baina aidiihim wa maa khalfahum. wa laa yuhithuuna bi shai-in min 'ilmihii illaa bi maashaa-a. wasi'a kursiyyuhu ssamaawaati wal arbhwa. wa laa ya-udhuu hifzhuhumaa wahuwal 'aliyyul adhwiiim."[Sema mara 1]

2.Utasoma Surat Ikhlaasw,Falaq na An-Naas ( x3 kwa kila surah moja)

✅Surah Al Ikhlaas

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيْمِ.
قُلْ هُوَ اللهُ أَحَـدٌ(ا). اَللّٰهُ الصَّمَـدُ(٢). لَمْ يَلِـدْ وَلَمْ يٌوْلَـدْ(٣). وَلَمْ يَكُـنْ لَهُ كُفُـوًا أَحَـد(٤)

Bismillahirrahmanirrahim,
1. Qul huwa allaahu ahad(un),
2. allaahu asw-swamad(u),
3. lam yalid walam yuulad(u),
4.walam yakullahu kufuwan ahad(un).

✅ Surah Al-Falaq

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيْمِ
قُلْ أَعُوْذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ، مِنْ شَرِّ ماَ خَلَقَ، وَمِنْ شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ، وَمِنْ شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ، وَمِنْ شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَد

Bismillahirrahmanirrahim,
1. Qul a'udhu birabbil falaq
2. Min sharri ma khalaq
3. Wamin sharri ghasiqin idha waqab
4. Wamin sharrin naffathaati fiil 'uqad
5. Wamin sharri haasidin idha hasad

✅Surah An-Nas

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيْمِ
قُلْ أَعُوْذُ بِرَبِّ النَّاسِ(١) مَلِكِ النَّاسِ(٢)
إِلَهِ النَّاسِ(٣
مِنْ شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ(٤)
اَلَّذِيْ يُوَسْوِسُ فِي صُدُوْرِ النَّاسِ(٥)
مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ(٦)

Bismillahirrahmanirrahim,
1. Qul a'uudhu birabbi nnaas,
2. Maliki nnaas,
3. Ilaahi nnaas,
4. Min sharri l-waswaasi lkhannaas,
5. Alladhii yuwaswisu fii swuduuri nnaas,
6. mina ljinnati wannaas

3. Dua of Protection
أَصْبَحْنَا وَأَصْبَحَ الْمُلْكُ لِلَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، لاَ إِلَـهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرُ. رَبِّ أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا فِيْ هَذَا الْيَوْمِ وَخَيْرَ مَا بَعْدَهُ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا فِيْ هَذَا الْيَوْمِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهُ، رَبِّ أَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ وَسُوْءِ الْكِبَرِ، رَبِّ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ عَذَابٍ فِي النَّارِ وَعَذَابٍ فِي الْقَبْرِ

"Asw-bahnaa wa asw-bahal mulku lillah walhamdulillah, laa ilaha illallah wahdahu laa sharika lah, lahul mulku walahul hamdu wa huwa ‘ala kulli shai-in qadir. Rabbi as-aluka khaira maa fii hadhal yaum wa khaira maa ba’dahu, wa a’udhu bika min sharri maa fii hadzal yaum wa sharri maa ba’dahu. Rabbi a’udhu bika minal kasali wa su-il kibar. Rabbi a’udhu bika min ‘adhabin fin naari wa ‘adhabin fil qabri."[Sema mara 1]

4. Dua submissive to Allah

اَللَّهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوْتُ وَإِلَيْكَ النُّشُوْرُ

Allahumma bika asw-bahnaa wa bika amshynaa wa bika nahyaa wa bika namuutu wa ilaikan nushuur."[Soma mara 1]

5. Dua sayyidul istighfar

اَللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّيْ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ أَنْتَ، خَلَقْتَنِيْ وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوْذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوْءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوْءُ بِذَنْبِيْ فَاغْفِرْ لِيْ فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوْبَ إِلاَّ أَنْتَ.

Allahumma anta rabbii laa ilaha illa anta, khalaqtanii wa anaa ‘abduka wa anaa ‘ala ‘ahdika wa wa’dika mas-tatea’tu. A’udhu bika min sharri maa swana’tu. Abu-ulaka bi ni’matika ‘alayya wa abu-u bi dhambii. Fagh-firlii fainnahu laa yagh-firudh dhunuuba illa anta."[Soma mara 1]

6. Dua of 'Afiat

اَللَّهُمَّ إِنِّيْ أَصْبَحْتُ أُشْهِدُكَ وَأُشْهِدُ حَمَلَةَ عَرْشِكَ، وَمَلاَئِكَتَكَ وَجَمِيْعَ خَلْقِكَ، أَنَّكَ أَنْتَ اللهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ أَنْتَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيْكَ لَكَ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُكَ وَرَسُوْلُكَ

Allahumma inni ash-bahtu ush-hiduka wa ush-hidu hamalata ‘arshika wa malaa-ikatak wa jami’a khalqik, annaka antallahu laa ilaha illa anta wahdaka laa shariika lak, wa anna Muhammadan ‘abduka wa rasuuluk. (soma mara 4)

7. Dua of salvation

اَللَّهُمَّ إِنِّيْ أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَاْلآخِرَةِ، اَللَّهُمَّ إِنِّيْ أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِيْنِيْ وَدُنْيَايَ وَأَهْلِيْ وَمَالِيْ اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِى وَآمِنْ رَوْعَاتِى. اَللَّهُمَّ احْفَظْنِيْ مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِيْ، وَعَنْ يَمِيْنِيْ وَعَنْ شِمَالِيْ، وَمِنْ فَوْقِيْ، وَأَعُوْذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِيْ

Allahumma innii as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyah fid dunyaa wal aakhirah. Allahumma innii as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyah fii diinii wa dun-yaya wa ahlii wa maalii. Allahumas-tur ‘awraatii wa aamin raw’aatii. Allahumma hfadh-nii mim bayni yadayya wa min khalfii wa ‘an yamiinii wa ‘an shimaalii wa min fawqii wa a'udhu bi ‘adhamatik an ughtala min tahtii.(Soma mara 1)

8. Dua of Protection
اَللَّهُمَّ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَاْلأَرْضِ، رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيْكَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَعُوْذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِيْ، وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطَانِ وَشِرْكِهِ، وَأَنْ أَقْتَرِفَ عَلَى نَفْسِيْ سُوْءًا أَوْ أَجُرَّهُ إِلَى مُسْلِمٍ

Allahumma ‘aalimal ghaybi wash shahaadah faatwiras samaawaati wal ardhwi. Rabba kulli shai-in wa maliikah. Ashhadu alla ilaha illa anta. A’udhu bika min sharri nafsii wa min sharrish shaytwaani wa shirkihi, wa an aqtarifa ‘alaa nafsii suu-an aw ajurrahu ilaa muslim.[Soma mara 1]

9. Dua avoids danger

بِسْمِ اللَّهِ الَّذِى لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَىْءٌ فِى الأَرْضِ وَلاَ فِى السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Bismillahil-ladhi la yadhwurru ma’asmihi shai’un fil ardhwi wa la fis-sama’i wa huwas-sami’ul aleem."[Soma mara 3]

10. Dua To Be Pleased
رَضِيْتُ بِاللهِ رَبًّا، وَبِاْلإِسْلاَمِ دِيْنًا، وَبِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَبِيًّا

Rabhwii-tu bil-lahi Rab-baaa, Wa bil-is-lami-deenaaa, Wa bi-muhammadin swal-lal-lahu alai-hi Wa-sal-lama Nabiy-yaaaan."[Soma mara 3]

11. Dua for help
يَا حَيُّ يَا قَيُّوْمُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيْثُ، وَأَصْلِحْ لِيْ شَأْنِيْ كُلَّهُ وَلاَ تَكِلْنِيْ إِلَى نَفْسِيْ طَرْفَةَ عَيْنٍ أَبَدًا

"Yaa Hayyu Yaa Qayyuum bi Rahmatika astaghiith Wa Aswlih lii sha’nee kullahu wa laa takilni ilaa nafsi twarfata ‘aynin abadan."[Soma mara 1]

12. Dua of Fitrah

أَصْبَحْنَا عَلَى فِطْرَةِ اْلإِسْلاَمِ وَعَلَى كَلِمَةِ اْلإِخْلاَصِ، وَعَلَى دِيْنِ نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَعَلَى مِلَّةِ أَبِيْنَا إِبْرَاهِيْمَ، حَنِيْفًا مُسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِيْنَ

Ash-bahnaa ‘ala fitwratil islaam wa ‘alaa kalimatil ikhlaasw, wa ‘alaa diini nabiyyinaa Muhammadin swallallahu ‘alaihi wa sallam, wa ‘alaa millati abiina Ibraahiima haniifam muslimaaw wa maa kaana minal mushrikin."[Soma mara 1]

13. Tasbih ,Tahmid
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ

"Subhan Allah wa bihamdihi."[Soma mara 100]

14. Tahlil
لاَ إِلَـهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرُ

Laa ilaha illallah wahdahu laa sharika lah, lahul mulku walahul hamdu wa huwa ‘ala kulli shai-in qadiir."[Soma mara 10 au 100]

15. Four phrases Heavier in the Scales
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ: عَدَدَ خَلْقِهِ، وَرِضَا نَفْسِهِ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ

"Subhanal-lahi wabihamdih, 'adada khalqihi waribhwa nafsih, wazinata 'arshih, wamidada kalimatih."[Soma mara 3]

16. Dua for beneficial knowledge, sustenance and good deeds
اَللَّهُمَّ إِنِّيْ أَسْأَلُكَ عِلْمًا نَافِعًا، وَرِزْقًا طَيِّبًا، وَعَمَلاً مُتَقَبَّلاً

Allahumma innii as-aluka ‘ilman naafi’a, wa rizqan twayyibaa, wa ‘amalan mutaqabbalaa.[Soma mara moja baada ya swala ya Alfajir]

17. Read istighfar

أَسْتَغْفِرُ اللهَ وَأَتُوْبُ إِلَيْهِ

"Astagh-firullah wa atuubu ilaih."[Sema mara 100]

18. Salawat(Durood) for Prophet Muhammad ﷺ

اللَّهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ عَلَى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ

Allahumma salli wa sallim alaa nabiyyina Muhammad.[Sema mara 10]

19. Protection of insect stings

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

"A'uwdhu bikalimaati Allaahit-taammaati min sharri maa khalaqa."[Sema mara 3]

20.Dua for sufficient and powerful reliance on Allah

حَسْبِيَ اللهُ لَآ إِلَهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ

"Hasbiyallaahu laa 'ilaaha 'illaa Huwa 'alayhi tawakkaltu wa Huwa Rabbul-'Arshil-'Adhwiim."[Sema mara 7]



Ukweli ni kwamba mahusiano yanakufa haraka si kwa sababu ya kukosekana kwa uelewano, mawasiliano na nia ya dhati pande z...
23/01/2026

Ukweli ni kwamba mahusiano yanakufa haraka si kwa sababu ya kukosekana kwa uelewano, mawasiliano na nia ya dhati pande zote mbili.

Hebu tuangalie kwa mizani ⚖️:

Kuna wanawake wanaochanganya mapenzi na biashara ❌

Lakini pia kuna wanaume wasiowajibika, wasiothamini, au wanaoahidi bila kutimiza ❌

👉 Tatizo kubwa si pesa, ni dhamira.

💡 Mahusiano ya kweli hujengwa kwa:
Heshima 🤝

Mawasiliano ya wazi 🗣️

Uwajibikaji pande zote mbili

Upendo unaoonekana kwa vitendo, si pesa pekee ❤️

Mwanamke kuhitaji msaada si kosa, na mwanaume kusaidia si kulipwa k**a kuna mapenzi ya kweli.
Lakini pale ambapo mapenzi yanakuwa masharti ya pesa, ndipo mahusiano yanapokufa haraka.

📌 Ujumbe wa msingi:
Mahusiano hayafi kwa sababu ya wanawake au wanaume,
yanakufa kwa sababu ya kukosa upendo wa kweli, uaminifu na malengo yanayofanana.✍🏽


`Kuna siku MOYO wako utapitia hali ya KUZIMIA...`_____Yaani, kuna mambo utakuwa unayapitia.....na NGUVU zitakuwa k**a zi...
18/01/2026

`Kuna siku MOYO wako utapitia hali ya KUZIMIA...`

_____Yaani, kuna mambo utakuwa unayapitia...
..na NGUVU zitakuwa k**a zimekuishia .

Na utaanza kuona MATUMAINI yanafifia.

Mara nyingi, siku k**a hizi hautaweza kulala vizuri kabisa.

Usingizi utapaa na itakuwa k**a wengi uliotamani wawe karibu nawe...
..wanakuwa MBALI nawe.

Hizi ni siku ambazo unatamani hata mtu akuulize “Unaendeleaje?”.

Bahati mbaya sana itaonekana k**a kila mtu yuko bize na mambo yake.

Wengi wamepoteza NDOTO zao katika kipindi hiki.

Wengi wamekata tamaa katika kipindi hiki.

Naomba nikukumbushe, hiki ni KIPINDI CHA MPITO...
..hakitadumu milele.

Hauko mbali na KUKIVUKA, na utakuja KUSHUHUDIA baadaye...
..kuwa MUNGU alikuvusha.

Usikate Tamaa, Usiishie Njiani.

K**a umependa makala hii tafadhali share na wengine.


 *Jumanne tarehe 13.01.2026**Siku 13/365*“Usipojitoa kufanya kazi kubwa juu ya kujijenga na kujitambua leo, kesho utajik...
13/01/2026


*Jumanne tarehe 13.01.2026*
*Siku 13/365*

“Usipojitoa kufanya kazi kubwa juu ya kujijenga na kujitambua leo, kesho utajikuta unaishi maisha yaliyopangwa na jamii badala ya ndoto zako.

Utakuwa ukifikiria wanavyofikiri wengine, ukitamani wanachotamani wengine, na kuogopa kuishi ukweli wako kwa sababu ya hukumu za watu.

Kufanya kazi juu ya nafsi yako ni kuvunja minyororo ya mawazo ya umati, ni kuchagua kuwa huru kuliko kukubalika, na ni kuthubutu kuishi maisha unayoyaongoza mwenyewe badala ya kuwa kikaragosi kinachovutwa na nyuzi za jamii.”

Maisha yetu k**a wanadamu mara nyingi k**a si zote tunadaiwa kuthubutu.

Kwenye safari ya kuthubutu kuna raha yake na maumivu yake. Raha ya kuthubutu huja tunapofanikisha jambo lakini maumivu ya kuthubutu huja tunaposhindwa jambo vilevile raha ya kuthubutu huja pale tunaposhindwa jambo lakini tukaamua kujifunza kupitia kushindwa kwetu.

Kuthubutu si jambo la kawaida linahitaji kujitoa sadaka na kukubali matokeo yatokanayo na kuthubutu ila kadiri tunapothubutu ndivyo tuvyojijenga kiakili na kihisia.

Mpendwa maisha hayatudai kushindwa kwetu bali yanatudai kuthubutu kwetu.

Maisha bila uthubutu ni sawa na kumeza tonge bila kulitafuna.

Address

Tanga
211XX

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Madam NeymaMhando posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category